<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>100</hymn_number>
<lyrics>[V1]
 Mbona washangaa njiani?
 Mbona warejea nyuma?
 Warudi tena gizani
 Alimokutoa Bwana?

[V2]
 Ni ya bure yote haya,
 Uliyofunzwa ya Mungu?
 Ni bure amekufia
 Bwana Yesu kwa uchungu?

[V3]
 Wamtia kristo aibu
 Na maneno yake pia?
 Siku yaja ya hesabu,
 Utamjibuje Bwana?

[V4]
 Upandapo tena hayo,
 Halafu utayavuna.
 Rudi kwa Bwana upesi,
 Mwombe akupokee tena.</lyrics>
<title>Tumrudie Bwana TZR100</title>
</song>